Msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja amesema kundi la Tip Top Connection bado lipo pale pale ila kutokana na umri na majukumu ni vigumu kuwa pamoja kama awali.
Dogo Janja amesema watu anaeleza kuwa kundi hilo limekufa kutokana hawatoi wimbo lakini haimaanisha limekufa.
“Tip Top ipo pale pale, umri na majukumu sio watu tena wa kukusanyana masikani tena ndio kitu ambacho watu wanakuwa wanapishana sana lakini Tip Top ipo na inafanya,” amesema.
“Watu wanazungumza kwa sababu hakuna wimbo wa kundi nahisi ndio chanzo cha watu kuzungumza hivyo,” Dogo Janja ameiambia Bongo5.
Ni kipindi kirefu sasa kundi la Top Top Connection halijaja na kazi ya pamoja. Msanii Madee aliwahi kueleza kuwa ndani ya kundi hilo kumezaliwa Manzese Music Baby (MMB) ambapo inawasimamia Dogo Janja na Gaza.