Thienry Henry uso kwa uso na Ufaransa yake kesho


Nusu fainali ya kwanza ya Fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi inatarajiwa kuchezwa kesho kwa kuzikutanisha timu za Ubelgiji na Ufaransa.

Kivutio kikubwa kesho ni juu ya uwepo wa nyota wa zamani wa Arsenal na Ufaransa, Thienry Henry ambaye ni kocha msaidizi wa Ubelgiji ambapo atakua anacheza dhidi ya timu yake ya Taifa, mashabiki wengi wanataka kujua kama Henry ataimba wimbo wa Ufaransa la.

Mchezo huo wa kwanza utakuwa  ni muhimu kwa makocha wa timu zote mbili , Roberto Martinez wa Ubelgiji na Didier Deschamps wa Ufaransa.

Kwa upande wa Kocha wa Ufaransa Deschamps ameweka wazi mkakati wake wa kutaka kuweka rekodi ya kushinda taji hili akiwa meneja baada ya kuiongoza Ufaransa kushinda taji hilo mwaka 1998 akiwa nahodha wa kikosi cha dhahabu.

Deschamps atapambana na mchezaji mwenzie aliyekua nae katika kikosi hicho cha dhababu mwaka 1998 wakichukua ubingwa wa dunia, Thiery Henry ambaye yupo kwenye benchi la ufundi la Timu ya Ubelgiji kwa sasa

Martinez kwa upande wake anaongoza kikosi chake ambacho kinatajwa kuwa na wachezaji wengi nyota katika historia ya soka la Ubelgiji.

Ubelgiji iliwaondoa Brazil katika hatua ya robo faainali kwa mabao 2-1 wakati Ufaransa iliinyuka Uruguay kwa mabao 2-0.
Mpya zaidi Nzee zaidi