Wadau wahamasisha michezo kwa watoto yatima


Na Ferdinand Shayo, Arusha.

Wadau wa michezo kutoka taasisi ya Who is Hussan wameandaa michezo ya mpira wa miguu ,michezo mbalimbali ya watoto kwa ajili ya kuhamasisha michezo Kwa ajili ya watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu ili kuvumbua vipaji vyao.

Mwakilishi wa taasisi ya who is Hussain, Tahera Sajan amesema kuwa kwa sasa wameyakumbuka makundi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ,walemavu na yatima ili kuchochea ari ya michezo kwani kundi hilo limekua likisahaulika katika masuala ya michezo.



Tahera amesema kuwa Michezo hiyo imewakutanisha watoto yatima kutoka mikoa ya Dodoma, Tanga,Kilimanjaro na Arusha lengo ikiwa ni kuwafanya wafurahi na kuhimiza ushiriki wao katika michezo.

Kwa upande wao watoto walioshiriki katika michezo hiyo William Damas amewaomba wadau wa michezo kuandaa michezo Hiyo Mara kwa mara ili kuibua vipaji vya watoto ambavyo vinaweza kuwa tinu kwa taifa..


Shaban Omary ni mtoto anaeleza kuwa wamefurahishwa na Aina mpya za michezo walizojifunza watawafundisha watoto wenzao

Mpya zaidi Nzee zaidi