BREAKING NEWS:: Mtatiro ajiuzulu CUF ajiunga CCM

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF Julius Mtatiro amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM huku akisema kuwa huu ni wakati wake wa kwenda kutumia vipaji vyake kikamilifu pia kuwa balozi mkubwa wa Rais Magufuli Ndani na nje ya Nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa jukwaa alilokuwa analisimamia katika siasa kwa miaka kumi limeshindwa kumpa nafasi yakuifanyie nchi yake maendeleo.