Dada wa Rais Magufuli afariki Dunia


Dada wa Rais John Magufuli aitwaye Monica Maguli amefariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Ikumbukwe jana Rais Magufuli alimtembelea dada yake huyo katika hospitali hiyo , lakini taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa leo imethibitisha kutokea kwa kifo hicho.