Haya ndio maamuzi ya Serikali kwa wakulima nchini


RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema Uchumi wa kati wa Tanzania ya Viwanda unaweza kufikiwa kama kutakuwa na uwekezaji katika sekta ya kilimo, Mifugo na Uvuvi na kwamba Maonyesho ya Wakulima Nanenane ni fursa kwa wakulima kupata na kujua teknolojia mpya.

Rais Mstaafu Mkapa amesema hayo, kwenye kilele cha sherehe ya 25 ya Wakulima, Nanenane ambazo zimefanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Aidha ameongeza kuwa ili wakulima waweze kunufaika na kilimo lazima kuwe na usimamizi bora hivyo Serikali imeondoa zuio la kuuza mazao nje ya nchi ili kutoa fursa soko na mapato kwa wakulima hivyo, wanaotaka kuuza mazao nje ya nchi watalazimika kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Uamuzi huo umetangazwa leo Agosti 8 na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alipokuwa akiyafunga rasmi maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani

"Hata hivyo, lazima kila mwananchi kuanzia ngazi ya kaya kuhakikisha uwepo wa akiba na usalama wa chakula," amesema Mkapa

Amewataka Watanzania kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo inayoajiri zaidi ya asilimia 65 ya watu nchini ili  kuvihakikishia malighafi viwanda vinavyoendelea kujengwa kutekeleza sera ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dkt Bashiru Ally akizungumza katika kilele cha maonyesho hayo anasema Mkoa Simiyu unaongoza Tanzania kwa viongozi wake kuwa na mshikamano, nidhamu na umoja na kwamba viongozi wake wanafanya kazi kwa ushirkiano, ambapo pia anasema Mkoa wa Simiyu unafuatiwa na Mkoa wa Singida, Dodoma na Pwani, huku Mkoa wa Mara, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam akiitaja kama mikoa ambayo viongozi wake hawana umoja na mshikamano na kuwataka kubadilika.

Naye, Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akizungumzia maonyesho hayo anaesema yatafanyika Mkoani Simiyu kwa miaka mitatu mfulilizo na kuitaka mikoa hiyo mitatu iliyoanda maonyesho hayo kuyageuza na kuyafanya yakimataifa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items