Naibu waziri wa nchi, ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI-Mhe.Joseph Kakunda, amesema serikali awamu ya tano inayoendeshwa na Dkt. John Pombe Magufuli,haitamvumilia wala kumfumbia macho mfanyabiashara yoyote ambae atadiliki kuingiza bidhaa kwa kutumia njia ya Panya kwa minajili ya kukwepa kulipa kodi.
Kakunda ameyasema hayo mbele ya mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, alipomtembelea ofisini kwake na kueleza kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakirudisha nyuma juhudi za serikali kwa kuingiza bidhaa kwa njia ya panya kitu ambacho hakiwezi kumvumilia mtu anaefanya hivyo ambaye anaikosesha serikali mapato.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amesema bidhaa zote zilizokamatwa na TRA zikiwemo sukari, mafuta, pamoja na maziwa ya unga vitagawiwa kwenye taasisi mbalimbali za serikali kama vile shule, kambi za wazee wasiojiweza, vituo vya watoto, hospitali.
