Serikali yatoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa kisa wakulima kukosa soko la kuuza Mahindi


Zaidi ya Tani Milioni moja na laki tatu za mahindi ya wakulima nchini yamekosa soko baada ya serikali kukosa mahali pa kuyauza hali ambayo inasababisha wakulima kupata hasara kwa kushindwa kurejesha gharama walizowekeza kwenye kilimo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ameyasema hayo wakati wa kilele cha sherehe za wakulima maarufu kwa jina la nane nane kanda ya nyanda za juu Kusini jijini Mbeya.

Baadhi ya wadau wa kilimo wamesema kuwa kutokana na wakulima kuanza kutumia mbegu na teknolojia bora za kilimo, uzalishaji wa mazao umeongezeka hivyo wanaiomba serikali kuongeza kasi ya kutafuta soko la mazao ya wakulima kwa kuwa ongezeko la uzalishaji wa mazao litakuwa likiongezeka kila mwaka, huku Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila akidai kuwa changamoto ya ubovu wa Miundombinu ya barabara vijijini inachangia mazao ya wakulima kukosa soko.

Akifunga maonyesho hayo, Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe. Joseph Kandege amewataka wakuu wa mikoa kuweka bidii ya kutafuta wawekezaji wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya wakulima ili iwe rahisi kuyapatia soko na pia kuwafanya wakulima wapate bei nzuri.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items