RAIS John Magufuli amefunga mjadala wa sakata la makontena 20 yaliyoagizwa kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, baada ya kuagiza yalipiwe kodi kwa kuwa yamebeba mali binafsi za kiongozi huyo na si za walimu.
Akizungumza jana na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato na watumishi wengine wa serikali Chato mkoani Geita, Rais Magufuli alisema Makonda alitaka kutumia walimu kujinufaisha.
“Ni lazima viongozi ‘no matter’ (haijalishi) uko kwenye ‘position’ (nafasi) tujenge mazingira ya kuwatumikia Watanzania, hizo ndizo sadaka zetu,” alisema na kuongeza:
“Umesikia sakata la Dar es Salaam eti Mkuu wa Mkoa ameleta makontena, ameambiwa alipe kodi, kwanini asilipe kodi?”
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Sheria ya Fedha, Sheria ya Madeni, Sheria ya Dhamana na misaada ya namba 30 mwaka 1974, kifungu cha tatu, sita, 10 na 13, 15 za nchi ni mtu mmoja ambaye ni Waziri wa Fedha aliyepewa dhamana ya kupokea misaada kwa ajili ya nchi, hakuna mwingine.
“Sasa ukichukua makontena kule, umezungumza na watu wengine na wafanyabiashara unasema una makontena yako halafu ukasema ni ya walimu wala hata shule hazitajwi,maana yake nini?”Alisema na kuongeza:
“Maana yake si unataka utumie walimu ulete makontena, utapeleka shule mbili tatu mengine unakwenda kuyauza unapeleka kwenye shopping mall, walimu walikwambia wanahitaji masofa au makochi? Wafanyakazi wasitumike kwa maslahi ya watu fulani.”
Baada ya kuzuiwa kwa makontena hayo mwanzoni mwa mwaka huu, Makonda aliishambulia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kwa kuyazuia bandarini.
“Nawashangaa kuanzia nyinyi wafanyakazi, bosi wenu wa TRA mpaka na waziri wenu wa fedha. Na mimi haya madude (makontena) yakibaki kwa sababu eti nimekosa kodi nitamwambia Rais,” alisema.
Machi 24, mwaka huu, Wizara ya Fedha na Mipango ilijibu barua ya Makonda yenye kumbukumbu namba FA.110/297/01/20, ya Januari 3, akiomba msamaha wa kodi kwenye samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam, zenye thamani ya takribani Sh. bilioni 1.4.
Barua ya wizara yenye kumbukumbu namba WFM/GEN/2018/19, ilieleza samani hizo ni msaada kutoka kwa wananchi wapenda maendeleo waishio Marekani.
“Baada ya kupokea maombi hayo nilitaka TRA kupitia sheria za kodi na kunishauri ipasavyo, nimepokea ushauri wa TRA kuwa sheria hazitoi msamaha wa kulipa ushuru wa forodha na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa serikali kuu na serikali za mitaa katika vifaa vilivyo katika maombi yaliyowasilishwa,” alisema.
Aidha, Mpango katika barua hiyo, alisema nyaraka zilizoko TRA kuhusiana na mzigo huo, zinaonyesha mmilikia/mpokeaji ni mtu binafsi, Paul Makonda na si taasisi au Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Hivyo basi kwa mujibu wa sheria, shehena hiyo ya samani haistahili kupata msamaha wa ushuru wa forodha/bidhaa na kodi ya VAT,” alisisitiza katika barua hiyo.
Jumamosi iliyopita, TRA iliaanza mnada wa makontena hayo katika bandari kavu ya DCID, yakiuzwa kwa Sh. milioni 60 kwa kontena na huku wateja wakifikia Sh. milioni 30.
Jumapili, Makonda akiwa katika ibada ya pili katika kanisa la Angilikana mjini Ngara mkoani Kagera, alimuomba Mungu asipatikane mteja wa makontena yake kwa kuwa yalikuwa ya kwenda kwa walimu.
“Alaaniwe mtu yule atakayenunua furniture (samani) za walimu. Nimefanya ibada maalum leo (juzi) ya kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa sababu naamini Mungu alinipa kwa ajili ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wanaofanya kazi katika mazingira magumu zikiwa ni jitihada zangu binafsi.”
“Hivi ni vifaa kwa ajili ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mungu hakunipa kwa ajili ya baa wala kumbi za starehe,” alisisitiza Makonda.
“Nakuhakikishia atakayenunua hivi vifaa vya walimu, amelaaniwa yeye na uzao wake na kamwe hatafanikiwa katika maisha yake. Nayasema haya nikiwa na uhakika kwa kuwa vya madhabahuni havichezewi,” alisisitiza.
Siku iliyofuata, Waziri Mpango alifanya ziara ya kushtukiza kwenye Bandari hiyo na kueleza kusikitishwa na kauli za kiongozi huyo na kuwataka Watanzania kuzipuuza na kwenda kununua mali hizo.
“Si sahihi kuingilia taratibu zilizowekwa na sheria za nchi na si kawaida yangu kulumbana kwenye mitandao, ndiyo maana nimeamua kufika hapa kuangalia kuna nini,” alisema.
“Sheria za nchi hazichagui sura wala cheo cha mtu na mimi ndicho nilichoapa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwa hiyo kamishna simamia sheria za kodi bila kuyumba,” alisisitiza.
“Napenda niwaombe viongozi wenzangu serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii, tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo,” alisema Dk. Mpango.
Wakati huo huo, Rais Magufuli aliwataka madiwani wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu matumizi ya fedha za bajeti, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha hizo zinaelekezwa katika miradi na huduma zenye kujibu kero na kuboresha maisha ya wananchi badala ya kuacha zikitumiwa kulipana posho za vikao na safari zisizo na tija.
“Nafahamu kuwa hata nyie madiwani huwa mnakaa kikao siku moja na mnataka kulipwa posho ya siku mbili au tatu, au mtumishi wa halmashauri anasafiri kwa siku mbili, lakini anaandikiwa posho za siku nne, nataka mchezo huu ukome, elekezeni fedha kwenye mahitaji muhimu ya wananchi, Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya simamieni hilo,” alisema.
Katika mkutano huo alianza kwa kupokea maswali, kero na maoni ya watumishi na viongozi, Rais Magufuli aliwahakikishia kuwa serikali imedhamiria kujenga uchumi wa kujitegemea na kutatua kero za wananchi wakiwamo wafanyakazi wote bila kubagua.