Mtu mmoja alietambulika kwa jina Zuwena Haji Mwadini (14) mkaazi wa kijijini Makunduchi amekutwa amejinyonga nyumbani kwao kwa kutumia mtandio .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 17-8-2018 majira ya 3:00 asubuhi huko kijijini makunduchi.
Kamanda Suleiman amemtaja marehemu huyo Zuwena Haji Mwadini ni mwanafunzi wa darasa la sita na huku akielezea chanzo cha tukio hilo ni ugomvi kati yake mtoto na mama yake na kuamua kujinyonga kwa kutumia mtandio.
Aidha Kamanda Suleiman ametoa wito kwa vijana kuwasikiliza wazazi wao pindi pale wanapotuasa kupitia mambo mbali mbali na huku akiwataka wazazi wawe karibu na watoto wao na kufanyana nao urafiki ili kuepusha vitendo hivyo vibaya.
Kwa upande mwengine Mtu mmoja nae ametambulika kwa jina la Mussa Khamis Juma (42) mkaazi wa Jang’ombe siku ya tarehe 11-8-2018 amekutwa na nyongo 8 huko Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja .
Kamanda Suleiman ametoa wito kwa wananchi wa vijiji hivyo kutoa ushirikiano na jeshi la polisi na kuwataka kulikataa jambo hilo na kuripoti makosa hayo ili kuhakikisha dawa za kulevya haziingii kwenye vijiji vyao