Priyanka Chopra aonyesha pete aliyovalishwa na mpenzi wake Nick Jonas


Ulikuwa unamtamani Priyanka Chopra? Basi pole sana mrembo huyo tayari ameshachukuliwa na kijana ambaye amemzidi kwa miaka 11.

Mrembo huyo ameonyesha hadharani pete ya uchumba ambayo amevalishwa na muimbaji wa Marekani Nick Jonas (25).


Kupitia picha iliyowekwa Jumanne hii kwenye mtandao wa Instagram na rafiki yake wa karibu, Raveena Tandon, Priyanka (36) ameonekana akiwa ameivaa pete hiyo inayodaiwa kuwa ya Almasi.

"Peecee and I getting our pouts in order ! 😂," ameandika Raveena kwenye picha hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi