RC Hapi agundua mapungufu Hospitali ya Rufaa, atishia kuifunga


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ametishia kuuvunja uongozi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa baada ya kubaini mapungufu mengi yanayosababisha malalamiko kutoka kwa wagonjwa wanaohudumiwa hospitalini hapo.

Hapi amesema kumekuwepo na malalamiko mengi ya wagonjwa wanaopata huduma kwenye hospitali hiyo ikiwemo kukosa dawa na pia wahudumu kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na kuagiza uongozi wa hospitali hiyo kushughulikia changamoto hizo haraka.