.

8/15/2018

Valencia ashangazwa na rafu aliyochezewa mchezaji wa Tanzania

Unaikumbuka rafu ambayo alichezewa Morris Abraham wa Tanzania kwenye kufuzu fainali za Africa kwa vijana waliyo na umri chini ya miaka 17 (U17)?
Basi kipande hiko cha video kimeonekana kusambaa sehemu kubwa ya ulimwengu - Mchezaji wa Manchester United, Antonio Valencia ameonyesha hisia zake juu ya kitendo hicho alichofanyiwa Morris na mchezaji wa Burundi.
Valencia ameweka video hiyo kupitia mtandao wa Instagram na kuandika maneno ambayo yanaonyesha kusikitishwa kwake kwa rafu hiyo huku akimtag beki mwenzake wa United, Eric Bailly.
"Jajajaj @ericbailly24😱😱😱," ameandika Valencia kwenye video hiyo. Katika mchezo huo wa huo wa kwanza wa kundi A, vijana wa Tanzania waliibuka na ushindi mabao 2 – 1 dhidi ya Burundi, mabao hayo yalifungwa na Kelvin John dakika ya 11 na Agiri Ngoda (dakika ya 29) wakati bao la Burundi likifungwa na Munaba Edson dakika ya 20.
Michuano hiyo ya kufuzu fainali za Africa kwa Vijana U17 imeanza Jumamosi ya Agosti 11 na kutarajiwa kufikia tamati Agosti 26, 2018.