Kaimu Katibu mkuu wa shirikiko la mpira wa miguu (TFF) Kidao wilfred amesema kuwa timu ya taifa ya Taifa Stars ina mechi dhidi ya Timu ya Uganda itakayochezwa mnamo Tarehe 8 mwezi wa tisa mwaka huu ambayo timu hizo zitachuana huko nchini Uganda ambapo katika michuano hiyo timu ya Taifa stars Itakuwa ugeneni.
Kidao ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za TFF zilizopo karume jijini Dar es salaam, vilevile amedai timu imefanya maandalizi makubwa ili timu iweze kufuzu michuano hiyo ili waweze kwenda nchini Cameroon kwaajili ya fainali za afrika.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.................USISAHAU KUSUBSCRIBE....................
