Wahandisi wawili wapigwa "STOP" Pwani, Waziri atoa siku 14 kukamilisha mradi


WAZIRI wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Mkuranga katika kukagua utekelezaji wa utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi na hakuridhishwa na utendaji wa baadhi ya wahusika katika idara hizo na kuamua kuwaweka kando ili wenye kasi watekeleze jukumu hilo.

Katika Ziara hiyo Kalemani  amemuagiza meneja Tanesco  mkoa wa Pwani kumsimamisha kazi  Mhandisi wa Mkoa na  pia amemuagiza meneja wa wilaya ya Mkuranga Mhandisi, Regina Mvungi kumsimamisha mhandisi mwenye dhamana hiyo katika wilaya ya Mkuranga kwa kushindwa kufanya kazi ya kuwasha umeme kwenye vijiji vilivyo kwenye mradi kata ya Vikundi.

Aidha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ametoa siku 14 Wilayani Mkuranga katika  kuhakikisha umeme unawaka katika vijiji vyote vilivyokatika mpango huo.Waziri hiyo aliyasema hayo Leo hii wakati wa ziara ya kutembelea wilayani Mkuranga ili kuona namna ya upatikanaji wa huduma ya Nishati ya Umeme katika Kata ya Kisiju,Vikindu na Tambani.

Kalemani amesema kuwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya pili haikufanya vizuri katika Tarafa ya Kisiju hivyo natoa siku 14 kuanzia kesho kuhakikisha umeme unawaka, aidha Kalemani ametoa  maagizo  kwa viongozi wa Tanesco katika ngazi ya Mkoa na Wilaya kuhakikisha umeme huo unawaka kwa wakati.

Naye Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Abdallah Ulega amesema  wananchi katika vijiji ambavyo vilitakiwa kupata umeme walikata minazi na miembe yao ili kupisha miundo mbinu ya umeme lakini ni zaidi ya miaka mitano tangu miundombinu ya umeme iwekwe na hakuna umeme.

Aidha Ulega amemshukuru Waziri Kalemani kwa ziara yake jimboni hapo kwani anaamini italeta mabadiliko na amewataka watendaji waliopewa maagizo na Waziri wayafanyie kazi mara moja
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items