Wakala wa Pogba amjia juu Scholes

Mino Raiola 

 Wakala Mino Raiola anayemsimamia kiungo wa klabu ya Manchester United Paul Pogba amezua mjadala kupitia mtandao wa Twitter baada ya kupandisha ujumbe unaomhusu kiungo wa zamani wa timu hiyo Paul Scholes.

Katika ujumbe wake huo Raiola anamtaka Scholes kuwa Mkurugenzi wa michezo wa Man United ili amshauri Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward kumuuza kiungo huyo raia wa Ufaransa.

Hatua hiyo imekuja wakati ambao kuna tetesi mbalimbali za nyota huyo mshindi wa Kombe la dunia 2018 kuwa hana furaha ndani ya klabu na anataka kuondoka. Scholes amekuwa akikosoa uchezaji wa Pogba ndani ya Man United kitu ambacho kinampa hasira Mino Raiola.

Baadhi ya wafuasi katika mtandao huo wanaoonekana kuwa ni mashabiki wa United wamemshambulia Raiola na kumtaka atafute timu haraka amuuze mchezaji wake.
 Paul Pogba


Mpya zaidi Nzee zaidi