DC Jokate amwagiwa pongezi na TAMWA


Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA), kimeeleza kufurahishwa na ushirikiano ambao kimepata kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na kueleza kuwa wanatamani iwe hivyo katika wilaya zingine 9 wanazofanya nazo kazi.

Mkurugenzi wa TAMWA, Edda Sanga, amesema wanafanya kazi katika wilaya 10, zikiwemo 7 za Tanzania bara na 3 za Zanzibar. Ameeleza kuwa watafanikiwa kudhibiti vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake endapo watapata ushirikiano kama waliopata wilayani Kisarawe.

''Tumefanikiwa sana wilayani Kisarawe ambayo ni kati ya wilaya 10 tunazofanya nazo kazi, Jokate alitupokea vizuri na tukaendesha shughuli zetu vizuri kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali yakiwemo madhehebu ya dini'', amesema Edda.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ameweka wazi kuwa zoezi la kumaliza ukatili kwa watoto na wanawake wilayani humo limeenda vizuri na maazimio yatatolewa siku ya mtoto wa kike duniani tarehe 11/10/2018.