Wizkid
Wizkid amethibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika “Kwa faida ndogo nitakayoipata kupitia ubia wangu wa kibiashara na Nike nitajenga shule nyumbani Lagos”.
Wizkid aliingia makubaliano ya kibiashara kupitia brand yake ya StarBoy na kampuni ya Nike ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vifaa vya michezo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

