Hiki ndicho kinachomsumbua Manara

 Baada ya kuenea kwa tetesi katika mitandao ya kijamii kuwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa club ya Simba SC Haji Manara anaumwa presha, Haji Manara mwenyewe ameweka wazi kinachomsumbua.

Haji Manara kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe unaoleza na kufafanua kwa kina kinachomsumbua kuwa ni food poison (Sumu ya kwenye chakula) sio presha wala ugonjwa wa moyo kama inavyoeleza.

“Siumwi pressure wala moyo kama inavyoandikwa mitandaoni..nahisi nimepata food poison na niwashukuru Madaktari walionihudumia awali Shinyanga na Mwanza ..now nisharejea Dar tayari kwa vipimo zaidi…Insha’Allah kila kitu kitazidi kuwa salama”