Huddah akataa kufananishwa na Vera Sidika


Mjasiriamali Alhuddah Njoroge, ‘Huddah Monroe’ amekataa kabisa kushiriki katika tuzo za Black Entertainment Film Fashion Television and Arts (BEFFTA) ambazo zinatarajiwa kufanyika mwezi huu nchini Uingereza, ambapo yupo kipengele cha International Film and Fashion ambacho hasimu wake Vera Sidika pia amechaguliwa kushiriki na kusema kuwa hawezi kulinganishwa naye hata kidogo.

Huddah ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii,

“Mmenichagua katika tuzo ambazo wala sizifuatilii kabisa nipo bize na mambo yangu na ninafanya mambo yanayonihusu na sipo kwa ajili ya kulinganishwa na hao mlioniweka nao, kwa Afrika sina wakulinganishwa naye yaani sijaona labda USA (Marekani), nipo bize na brand yangu ya HUDDAH na kuangalia vipi naikuza sitaki ushindani na mtu,” aliandika Huddah.