Huu ndio muonekano wa duka la Wema Sepetu

Miss Tanzania 2006 na muigizaji Wema Sepetu amerudi tena kwenye headlines baada ya wengi kudai kuwa anakaribia kufungua duka lake mwenyewe lenye jina la “Little sweethearts” hivi karibuni.

Tetesi hizo zimezuka baada ya Wema Sepetu kuonekana akiwa ameenda China na baadhi ya videos zikimuonyesha akiwa anarudi Tanzania huku akiwa na mizigo mingi  ambayo inasadikika ni kwaajili ya biashara.

Duka hilo linadaiwa kuwa litakuwa likiuza nguo za watoto na huku baadhi ya picha ya muonekano wa duka hilo limesambaa kwenye mitandao ya kijamii, marafiki wa karibu wa Wema Sepetu wameonekana pia kumpongeza kwa jitihada hizo kurasa zao za instagram.