Korea Kaskazini yakubali kufunga kituo cha Nyuklia, yaipa Marekani masharti


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameahidi kukiteketeza kituo Kikuu cha nyuklia cha  Tongchang-ri na badala yake kuanzisha kituo cha kurushia mizinga katika eneo hilo baada ya mazungumzo na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliowakutanisha na  kiongozi wa Korea kaskazini, rais wa Korea Kusini Moon Jae-In amesema baada ya mkutano uliofanyika Pyongyang ,kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Hong Un amekubali kukifunga kinu cha Tongchang-ri na kufungua kituo cha mizinga kwa usimamizi wa nchi washirika.

Hata hivyo kiongozi wa Korea Kaskazini amesema atakifunga kinu cha nyuklia cha Nyongbyong iwapo Marekani itayafanyia kazi makubaliano waliyowekeana.