Mengi akubali kuilea Serengeti Boys, atamba kumkabidhi Rais Magufuli kombe


Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi amekubali kuwa mlezi wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys.

Akiongea mbele ya Rais Wa TFF na makamu wake Dk Mengi amesema amekubali ulezi huo.

Amesema ana imani Timu hiyo itachukua kombe na kumkabidhi Rais Dk John Pombe Magufuli.