Nchi za SADC kuimarisha upatikanaji wa Nishati


Na Ferdinand Shayo, Arusha
Wataalamu wa Masuala ya Nishati kutoka  Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wamekutana jijini Arusha kujadili upatikanaji endelevu wa nishati mbalimbali katika nchi hizo na kuangalia namna ya kufanya biashara kwa nchi mwanachama ili kutatua tatizo la uhaba  wa nishati .

Meneja Miradi Tanesco Steven Manda amesema kuwa wamekutana na nchi hizo na kuangalia jinsi ya kuhakikisha kuwa nishati endelevu inapatikana katika nchi hizo .

Meneja Udhibiti wa nishati nchini Switzerland ,Wilson Masango amesema kuwa nchi za Afrika zinapaswa kufikiri kuuziana umeme unaozalishwa ili kuziba pengo kwa nchi zenye uhaba wa nishati.

Mkurugenzi Mtendaji  wa kampuni ya Songas ,Nigel Whittaker amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na Tanesco ili kuhakikisha kuwa watanzania wanapata nishati kwa garama nafuu
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items