NA TIMOTHY ITEMBE TARIME.
KIONGOZI wa mbiu za mwenge kitaifa 2018,Charles Kabeho ameunga mkono kauli ya a Rais wa jamuhuri ya muungano ya Tanzania,John Pombe Magufuli kuwa Tarime inamaendeleo makubwa kufuatia kuundwa mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya.
Magufuli alisema hayo siku chache zilizopita wakati alipokuwa Tarime kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo alisema kuwa Tarime ni moja ya mji inayokuwa kwa kasi kimaendeleo baada ya kuacha tabia ya mapigano ya koo iliokuwepo hapo nyuma kabla ya kuundwa kwa mkoa wa kipolisi.
“Nawapongeza watu wa Tarime kwasababu ya maendeleo yaliyopo ni mji unakuwa kwakasi baada ya kuacha mapigano ya koo ambayoyalikuwepo kabla ya kuundwa mkoa wa kipolisi na mapigano hayo yalikuwa yanarudisha maendeleo nyuma”alisema Magufuli.
Kupitia nafasi iliyopo ya Amani Tarime mmejenga majumba bora ya kisasa kwaajili ya kuwekeza na vijana wanapata ajira kwa hali hiyo nawaomba muendelee kudumisha amani asitokee mtu anavuruga amani hiyo vinginevyo tutamshugulikia liongeza kusema.
Kauli hiyo ilionyesha kuungwa mkono na kiongozi wa mbiu za mwenge kitaifa 2018,Charles Kabeho wakati akifungua na kuweka jiwe la msingi katika hoteli ya RMM INVESMENT HOTEL iliyopo mji wa Sirari mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Kenya.
“Nimefurahishwa na wakekezaji wa ndani hususani mmiliki wa hoteli ya RMM INVESTIMENT kwasababu amefanya kitu kizuri hoteli hii itaenda kutoa ajira kwa wazawa na kulipa mapato ndani ya halimashauri ili kukuza uchumi wa halmashauri na Taifa kwa ujumla”alisema Kabeho.
Kabeho pia alifungua jengo la Busnes Cente lililopo Tarime pamoja na Kituo chakuweka Mafuta PKM ambacho kimeajiri watu 10.
Akisoma taarifa kwa kiongozi wa mbiu za mwenge Kitaifa mmiliki wa RMM Raphael Mwita Mseti alisema kuwa Sirari wanakabilia na uhaba wa maji pamoja na huduma za mawasiliano ya mitandao ya Vodacom na mitandao mingine ya kitanzania badala yake wanatumia kwa wingi mitandao kutoka nchi jirani ya Kenya na kuwa kwahali hiyo wanapata usumbufu wa mawasiliano pamoja na maji ya kutumia safi na salama.
“Ujenzi wa hoteli hii umekamilika na sasa tunaendelea na hatua ya uwekaji samani ambapo umetugarimu kiasi cha shilingi 499746500 mradi huu wa hoteli utakuwa na manufaa kwa serikali na jamii kwa ujumla kuongeza mapato ya serikali kuu kupitia kodi mbalimbali na kutoa ajira kwa Wazawa 55 wakiwemo wafanyabiashara wajasiriamali wadogowadogo”alisema Mseti.
Mwenge huo wa Uhuru ukiwa halmashauri ya Tarime vijijini na Tarime Mjini mkoani Mara ulizindua miradi 13 yenye garama ya shilingi zaidi ya bilioni 5 ambapo miradi yote imekidhi vigezo kwa mjibu wa mkuu wa wilaya Tarime,Glorius Luoga pamoja na wakurugenzi wake,App Tindwa na Elias Ntiruhungwa wa halmashauri ya Mji wa Tarime.

