Na Ferdinand Shayo ,Arusha.
Wilaya ya Karatu ina wanafunzi 2000 wasiojua kusoma na kuandika ambao wako katika ngazi ya darasa la kwanza hadi la tatu.
Aidha Idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu ni 22,015 wanaojua kusoma ,kuandika na kuhesabu in 20,013 wasiojua kusoma na kuandika ni 2002.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya kusoma duniani yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la world vision ambapo amesema kuwa juhudi zinahitajika ili kupunguza tatizo hilo.
Bi.Mahongo amesema kuwa uanzishwaji wa kambi za kusoma utasaidia wanafunzi kuimarika katika stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu.
Kaimu Meneja mradi wa dream village ulioko chini ya shirika la World Vision ,Richard Kitomari Wilaya ya Karatu amesema kuwa shirika hilo linatekeleza mradi wa kukuza stadi za kusoma kupitia makambi yaliyoanzishwa katika vijiji Dumbechan ,Mbuga nyekundu ,Jobaj pamoja na ujenzi wa madarasa ,nyumba za walimu na vyoo ili kuboresha maisha ya watoto .
Kwa upande wake mwanafunzi aliyenufaika na kambi hizo Izack Samweli amesema kuwa wameweza kujifunza kusoma ,kuandika na kuhesabu kwa kwa kutumia vizuri muda wa ziada kujisomea kwenye makambi hayo.
