Serikali yatangaza kiama cha wanaovua Pomboo


Na.Thabit Madai, Zanzibar
Idara ya Maendeleo na Uvuvi Zanzibar imesema itahakikisha inawatafuta na kuwapatia adhabu kali wavuvi waliohusika na kuvua samaki aina ya pomboo 4 katika  Eneo la ghuba ya chwaka mkoa wa kaskazini Unguja.

Akitoa taarifa kwa kamati za uvuvi ya Chwaka na kizimkazi Mkurugenzi wa Idara hiyo Mussa Abudu Jumbe alisema idara hiyo itaendelea kuwatafuta wavuvi pamoja na watu wote waliohusika katika kuwavua pamoja na kuwauza samaki hao  4 aina ya pomboo Eneo la chwaka na kizimkazi.

“ Kwa mujibu wa sheria ni marufuku kwa mtu yoyote kuvua samaki aina ya Pomboo, kasa, nguva pamoja na nyangumi hii kutokana na samaki hao kuwa mbioni kutoweka pamoja na kuwa wachache” alisema mkurugenzi wa Idara hiyo.

Aidha alisema  kutokana na kosa hilo lililofanywa na wavuvi wa ghuba ya chwaka  kinyume na sheria za idara ya uvuvi hatua kali za sheria zitazchukuliwa ikiwemo kutozwa faini au kifungo kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja mara baaada ya kukamatwa.

Hata hivyo aliipongeza  kamati ya  uvuvi ya kizimkazi kwa kutoa mashirikiano  juu ya uhujumu wa samaki hao na kuhakikisha wanamnusuru Yule aliyekua hai kwa kumrejesha baharini na kuwataka wananchi kuzipza mashirikiano kamati za uvuvi ili mkuweza kuzipa nguvu katika kuhifadhi mali za baharini.