Inatajwa kuwa mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ni ya pili kwa hadhi na umaarufu katika soka duniani baada ya ile ya kombe la dunia. Kwa mujibu wa takwimu za UEFA, watu 380 millioni kutoka nchi takribani 200 walitazama fainali ya msimu uliopita ya klabu bingwa Ulaya kati ya-
Liverpool na Real Madrid.
Michuano hiyo iliyo na wafuasi zaidi ya 150 millioni ulimwenguni kote, inarejea tena hii leo kwa michezo nane kupigwa katika hatua ya makundi huku michezo inayovuta hisia za wengi ni mchezo wa Liverpool wanaoikaribisha PSG na Inter Milan iliyorejea katika michuano hiyo baada ya misimu kadhaa itakapopambana na Tottenham Hortspurs.
Liverpool na PSG zimewahi kukutana mara mbili hapo kabla katika hatua ya nusu fainali ya kombe la washindi Ulaya msimu wa 1996/97, ambapo kila timu iliibuka na ushindi mara moja lakini PSG ilisonga mbele kwa uwiano wa mabao 3-2.
Kwa Liverpool, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwao kukutana na timu kutoka Ufaransa tangu msimu wa 2009/10 ambapo ilifungwa 2-1 na Lyon katika dimba la Anfield kabla ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano ugenini. Na kwa upande wa PSG, imecheza michezo minne ya hivi karibuni bila kupata ushindi dhidi ya timu za Uingereza, ikifungwa mitatu na kutoka sare mchezo mmoja.
Kwenye michuano ya Ulaya msimu uliopita, Liverpool iliweka historia ya kuwa na wachezaji watatu waliofunga mabao 10 kila mmoja, ambapo Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino ndiyo wafungaji wa magoli hayo, huku Edinson Cavani wa PSG akiwa amefunga mabao nane katika mechi 14 alizokutana dhidi ya klabu za Uingereza.
Katika mchezo wa Inter Milan na Spurs, timu hizo zinakutana kwa mara ya tano katika michuano hiyo huku kila timu ikishinda michezo miwili kati ya hiyo waliyokutana na ushindi huo ukiwa katika viwanja vyao vya nyumbani.
Mara ya mwisho kwa Spurs kucheza na Inter Milan ni katika hatua ya makundi msimu wa 2010/11 ambapo Spurs ilifungwa mabao 4-3 ugenini, mchezo ambao Gareth Bale alifunga ‘Hat-Trick’ kabla ya kushinda 3-1 katika mchezo wa nyumbani.
Spurs imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo nane ya ugenini katika michuano ya ulaya dhidi ya timu za Italia, ikifungwa mechi nne na nne zikiisha kwa sare. Mchezo pekee iliyoshinda ni dhidi ya AC Milan katika dimba la San Siro, bao ambalo lilifungwa na Peter Crouch.