Lukuvi auvaa mgogoro wa Mkuyuni, Uwanja wa Ndege

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na maendeleo na makazi,Wiliam Lukuvi ameagiza mmiliki wa eneo linalojengwa shule ya msingi Buguti katika kata ya Turwa iliyopo halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kurudisha hati ya eneo hilo ndani ya siku mbili vinginevyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na jeshi la polisi.

Waziri huyo alitamka leo katika mkutano a hadhara alipokuwa akisikiliza kero mbalimbali za migogoro ya Ardhi uliofanyikia  viwanja vya shule ya Msingi Sabasaba iliyopo katika halmashauri ya Mji wa Tarime.

"Nimeagiza hati hiyo iridishwe kufikia Septembe 20 vinginevyo mmiliki wao Eneo hilo Magaria Manko kama hatarudisha ndani ya siku nilizosema atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na kufikishwa polisi"alisema Lukuvi.

 Lukuvi alitumia nafasi hiyo kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo Elias Ntiruhungwa kwa kushirikiana mkuu wa wilaya Tarime,Glorius Luoga kuandaa mpango wa ushirikishwaji Wananchi ili kuendeleza ujenzi wa shule hiyo na watoto kuanza masomo.

Pia Waziri huyo aliongeza kuwa wananchi wanaofanya biashara za ndizi mbichi kuandalia waeneo ya kuuzia bidhaa zao badala ya kukaa kwenye jua wakipigwa mavumbi na jua.

"Haiwezekeni mkakusanya ushuru lakini wafanyabiashara wenu wakaendelea kufanyia biashara zao maeneo ambayo hayaridhishi naagiza halmashauri hii kuwaandalia wafanyabiashara maeneo mazuri ya kufanyia biashara zao kwa raha msitarehe na hilo niagizo kutoka kwa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuwa wafanyabiashara waandaliwe maenel mazuri ya kufanyiabiasharazao "alisema Lukuvi.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo alisema kuwa atahakikisha wanatenga bejeti ya kuwaandalia maeneo ya wafanyabiashara wa ndizi mbichi ili kuwajengea eneo la kivuli cha kujisitiri pindi wanapokuwa wanafanyabiashara zao.

Baadhi ya wananchi katika eneo hilo walimwambia Waziri huyo kuwa tangu mmiliki huyo alipomilikishwa eneo hilo mwaka 1985 hajawahi kuendeleza eneo hilo na pia hajawahi kulipia kodi eneo lake hilo miaka hiyo yote.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items