Wafungwa na wagonjwa wamwagiwa misaada Lindi


Na. Ahmad Mmow, Lindi.

KATIKA kutekeleza maamrisho ya dhehebu na dini Jumuia ya Khoja Ithaasheri Jamaat ya Lindi, leo imekabidhi msaada kwa gereza la wilaya ya Lindi kwa ajili ya wafungwa na wagojwa waliopo katika hosiptali ya rufaa ya mkoa wa Lindi (Sokoine).

Akikabidhi msaada huo Katibu wa jumuia hiyo, Mahmood Dhalla kwa nyakati na maeneo tofauti, kwa Kaimu mkuu wa gereza hilo na muuguzi mfawidhi wa hosipitali ya Sokoine alisema msaada huo ni utekelezaji wa maagizo ya dini ya kiislam katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa mtume Muhmmad S.W.A (Hussein) aliyeuwawa Karbala nchini Irak miaka 1440 iliyopita.

Alisema miongoni mwa maamrisho hayo nikusaidia wenye shida na uhitaji maalum katika kila mwanzoni mwa mwaka wa kiislam unaojulikana kama muharrami, ambapo mwaka huu waliamua kupeleka vifaa mbalimbali katika gereza na hosipitali ili  vitumiwe na wafungwa na wagonjwa.

Katibu huyo wa jumuia alivitaja baadhi ya vifaa, vipodozi na vyakula ambavyoni  pamoja  sabuni zakuogea, nyembe, sabuni za kufulia, dawa za meno, miswaki, maji, juisi, taulo na poda huku akiweka wazi kwamba thamani ya vitu hivyo ni shilingi 945,000.

Kwaupande wake kaimu mkuu wa gereza hilo, Mrakibu msaidizi wa magezeza(ASP) Peter Mbele  licha ya kushukuru kwa msaada huo, alitoa wito kwa viongozi wa dini kutembelea na kwenda kutoa nasaha na kusaidia wafungwa.

" Tunawahitaji kwa ajili ya kusaidia kurekebisha tabia za wafungwa.Kwahiyo kitendo mlichofanya nikuisaidia serikali kurekebisha tabia za wafungwa,"alisema Mbele.

Aidha kaimu mkuu huyo wa gereza la Lindi alitoa wito kwa viongozi wa dini kusaidia pia vifaa vya kufanyia ibada.Ikiwamo mikeka.Kwani baadhi ya wafungwa wanafanya ibada gerezani humo.

Nae muuguzi mfawidhi wa hospitali ya Sokoine, Edisa Mtondonjele, alitoa wito kwa jamii ikiwamo taasisi za dini, mashirika ya kiraia na wafanyabiashara kujenga mazoea ya kutembelea hospitali ili kuona na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wagonjwa.

Aliweka wazi kwamba baadhi ya wagonjwa wanashndwa kumudu gharama za msingi kwasababu ya uwezo mdogo wa kiuchumi.Kwahiyo wakitembelea itakuwa rahisi kuwasaidia.