Waziri Mhagama awataka walimu kutekeleza hoja za CAG


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amewaagiza wajumbe wa baraza la chama cha walimu Tanzania kutekeleza hoja zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Hayo ameyasema hii leo wakati wa kikao cha dharura kilichowakutanisha wajumbe hao kujadili hoja zote zilizotolewa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) katika taarifa yake ya mwaka 2016/2017.

Waziri Mhagama alieleza kuwa ripoti ya CAG imeelezea changamoto zilizokuwepo kwenye chama hapo awali ikiwemo masuala ya mapato na matumizi ya chama, mfumo wa uongozi na uwajibikaji, mikataba iliyoingiwa na chama ya uwekezaji, suala la utozaji ada kwa wananchana na mfumo wa sera ya malipo ya fedha.

“Wajumbe wa baraza hili mkishiriki kikamilifu katika kujadili na kufikia maamuzi ya pamoja ili kutimiza malengo ya chama na kutakuwa na utaratibu utakaosaidia kuongeza uwazi na mshikamano miongoni mwa wanachama” alisisitiza Mhagama.

Aliongeza pia kwa kuyatekeleza hayo chama kitakuwa na utaratibu mzuri utakaoheshimiwa na kila kiongozi wa chama na wanachama wote pamoja na namna bora ya kutunza na kutumia fedha za chama ili ziweze kutumika katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa manufaa ya wanachama wote.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items