Wema Sepetu avuruga ratiba nzima ya Twanga Pepeta


TAMASHA la kihistoria la kuadhimisha miaka 20 ya Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, lililopangwa kufanyika Septemba 29, mwaka huu, limesogezwa mbele kwa sababu zisizoweza kuzuilika.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka, alisema wameamua kulisogeza mbele tamasha hilo hadi Oktoba 6, mwaka huu lakini pia wamebadilisha ukumbi wa kufanyia tamasha hilo.

Alisema, badala ya kufanyika The Legends Club, sasa litafanyikia katika ukumbi wa The Life uliopo Mwenge.

“ Tumebadilisha siku ya kufanya tamasha kwa sababu ya kupisha matukio ambayo yatakuwa yanafanyika siku za karibuni za tamasha hilo.

“Kwanza tumeamua kumpisha Wema Sepetu na sherehe yake ya kuzaliwa ambayo itafanyika Septemba 28, na mechi ya watani wa jadi, tunafahamu wapenzi wa muziki wetu ndiyo mashabiki wa Wema, ndiyo wapenzi wa mpira pia, kuliko kuwarundikia burudani wakati mmoja bora sisi tusogee mbele na kuwapa nafasi kuhudhuria ‘events’ hizo nyingine,” alisema Asha Baraka.

Asha aliongeza kwamba sababu za kubadilisha ukumbi ni kupeleka tamasha hilo kwenye ukumbi mkubwa zaidi kutokana na mwamko kuwa mkubwa na kuonekana pale The Legends Club hapatatosha.   
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items