Mabeho agoma kufungua majengo ya Milionii 30


Na Timothy Itembe, Rorya
KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa 2018, Charles Mabeho jana amegoma kufungua mradi wa madarasa matatu yenye thamani ya shilingi milioni 30 wilayani Rorya mkoani Mara kwa madai kuwa mradi huo haulingani na fedha zilizotumika.

Mwenge huo wa Uhuru  katika halmashauri ya Rorya umezindua  miradi mingine saba ambapo Mabeho alikataa kuzindua mradi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Chereche.

Mkuu wa wilaya ya Rorya Saimoni Chacha amesema kuwa kukataliwa kwa mradi huo ni baada ya kiongozi wa mbio hizo kubaini kuwa garama ya mradi hailingani na uhalisia wa mradi.

Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa vyumba vinne vya madarasa Kijiji cha Ochuna wenye gharama ya shilingi milioni 88 fedha kutoka serikali kuu, mradi wa kisima cha maji kijiji cha Irienyi wenye dhamani ya shilingi milioni 19 fedha kutoka serikali kuu, kilimo cha umwagiliaji cha kisasa cha migomba katika  kijiji cha kinesi wenye gharama ya shilingi milioni 15.

Miradi mingine ni pamoja na mradi wa kikundi cha vijana Nyota Njema wa kijiji cha Kinesi ambapo walikopeshwa fedha na halmashauri shilingi Laki Saba.

Naye Mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo amesema amejitahidi kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na mradi wa darasa angalau moja alilojenga kwa kutumia nguvu zake ambapo katika kila darasa alikuwa akitumia gharama ya shilingi milioni 12 hadi shilingi milioni 13.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items