RC Mongella atoa onyo kali kwa wanaokeketa wasichana


Na James Timber, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka wananchi kuepukana na mila potofu huku akisema Serikali haitomvumilia mtu yeyote ambaye atakiuka sheria za nchi sambamba na kufanya vitendo vinavyoashiria uvunjaji wa haki za binadamu.

RC Mongella amesema kitendo cha kuharibu kiungo cha binadamu yeyote ni kuvunja sheria huku akizitaka taasisi mbalimbali ikiwemo za Dini kushirikiana kuhakikisha wanapiga vita vitendo vya ukeketaji.

Jamii mbalimbali zimekua zikiwafanyia tohara watoto wa kike kwa kigezo cha kuwafundishe maadili na sasa Mongella anatoa rai kwa wananchi kuepukana na mila hizo ambazo licha ya kwenda kinyume na haki za binadamu lakini pia zina madhara mengi ya kiafya.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items