F Zijue Njia mbadala Wa Kujitibu Maumivu Ya kichwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Zijue Njia mbadala Wa Kujitibu Maumivu Ya kichwa


Endapo kichwa chako kinakusumbua mara kwa mara na umekuwa huelewi ufanye nini basi makala hii inakuhusu kwani leo nitazungumzia vitu ambavyo vitakusaidia kuweza kujitibu tatizo hilo;

1. Tumia tangawizi.
Tangawizi inajulikana kama dawa nzuri kwa kutibu maumivu ya kichwa. Inachofanya tangawizi ni kupunguza maambukizi kwenye mishipa yako ya damu.

Kuna namna mbili unaweza kutumia tangawizi kutibu maumivu ya kichwa.
Moja ni kutengeneza juisi ya tangawizi, kipande kidogo tu cha tangawizi tumia maji na blenda tengeneza juisi yake upate kikombe kimoja na uchuje kisha ongeza vijiko vikubwa viwili vya maji maji ya limau na asali kidogo kupata radha na unywe kutwa mara 1 kwa siku kadhaa mpaka maumivu yameisha.

Namna ya pili ni kutengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi, maji na asali kama ndiyo sukari yako.

Kunywa chai hii kikombe kimoja kutwa mara 1 au 2 kwa siku kadhaa.

Unaweza pia kutafuna kipande kidogo cha tangawizi kupunguza maumivu hayo.

Tangawizi isitumike kwa wingi kwa mtu anayetafuta ujauzito au mwenye mimba changa.

2. Kipande cha barafu
Barafu ni aina nyingine ya dawa ya asili isiyo na gharama ya kutibu maumivu ya kichwa. Kipande cha barafu kinasaidia kupunguza muwako au joto vitu ambavyo ni moja ya vitu vinavyoweza kusababisha maumivu ya kichwa.

3. Barafu pia ni nzuri kurekebisha hali ya maumivu.
Unaweza kutumia kipande cha barafu kuondoa maumivu ya kichwa kwa namna hizi mbili zifuatazo:

Kwanza weka kipande cha barafu katika kitambaa kisafi na uweke nyuma ya shingo yako kwa dakika kadhaa. Hii njia itakuondolea maumivu haraka sana.

Namna nyingine ni kuweka kitambaa safi ndani ya maji ya baridi sana kama barafu kisha funika sehemu ya mbele ya kichwa chako na kitambaa hiki kwa dakika 5. Unaweza kufanya zoezi hili mara kadhaa kwa siku mpaka maumivu yamepotea.

4. Mrehani
Unaamini kuwa mrehani (basili) unaweza kukusaidia kuondoa maumivu yako ya kichwa kwa haraka? Hii ni kwa sababu sifa ya kutuliza maumivu (analgesic properties) ipatikanayo kwenye mrehani inaweza kusaidia kutuliza kichwa chako.
Kutibu maumivu ya kichwa kwa kutumia mrehani tumia njia zifuatazo:

Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha ipua na tumbukiza majani matatu mpaka manne ya mrehani na uache kwa dakika kadhaa.

Ongeza asali kidogo kupata radha kisha kunywa chai hiyo ili kuondoa maumivu ya kichwa.
Unaweza pia kuchemsha hayo maji sambamba na majani ya mrehani ndani yake kama unavyofanya kupika chai nyingine ya kawaida.

Au unaweza pia kutafuna tu majani kadhaa ya mrehani moja kwa moja mabichi hivyo hivyo mara kadhaa kwa siku. Unaweza pia ukipata mafuta ya mrehani ukapakaa kwenye paji la uso mara kadhaa kwa siku ili kuondoa maumivu haya ya kichwa.

Uchaguzi ni wako.
Hizo zote hapo juu ni dawa za asili za kuondoa maumivu ya kichwa ambazo unapaswa kuzijaribu.

5. Karafuu
Kwa vile karafuu ina sifa ya kukufanya mtulivu na kukuondolea maumivu mbalimbali basi ninaiandika hapa kama dawa ya asili unayoweza kuitumia kuondoa maumivu yako ya kichwa ambayo unatakiwa uijaribu pia.
Hivyo unaweza kutumia karafuu kuondoa maumivu yako ya kichwa.

Tumia kwa namna zifuatazo:
Kwanza chukua karafuu kadhaa na uzitwange kidogo ila zisiwe unga, kisha zifunge kwenye tishu. Muda wowote kichwa kikiuma sogeza karibu na pua yako na unusenuse mara kadhaa mpaka maumivu yametulia.

Namna nyingine ni kuchukua mafuta ya karafuu na ufanye masaji ya kichwa ukitumia mafuta haya.

Unaweza pia kuchanganya matone mawili ya mafuta ya karafuu, kijiko kidogo kimoja cha chai cha chumvi na vijiko vidogo viwili vya mafuta ya nazi. Tumia mchanganyiko huu kufanya masaji ya kichwa na ya paji la uso kuondoa maumivu ya kichwa.

Tumia njia hizo ukitumia karafuu kutibu maumivu yako ya kichwa.

Endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.