10/11/2018

Ali Kiba ashindwa kuvumilia, afunguka ujauzito wa Mke wake


AMEVUNJA ukimya! Supastaa wa Bongo fleva, Ali Kiba amefunguka kuhusu uvumbi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya ujauzito wa mke wake.

Hitmaker huyo wa ngoma ya mvumo wa radi amesema mke wake hana ujauzito kama watu wanavyoeneza huku akisema tetesi hizo zilianza baada ya kusambaa kwa picha ya mke wake akiwa amevaa koti kubwa.

" Hakuna chochote ni uzushi tu huo wa watu, unajua alipiga picha amevaa koti sasa likawa limetunishwa na upepo ndio ikawa shida hapo kila mtu mitandaoni akaanza kuongea lake lakini kiukweli mke wangu hana ujauzito," amesema Kiba.

Kiba ambaye ametambulisha wimbo mpya sambamba na wasanii kutoka lebo yake ya Kings Music amefunguka pia kuhusu kutoonekana mara nyingi na mke wake akisema ni kwa sababu mkewe ni msomi ambaye yupo busy sana na majukumu yake ya kazi lakini pia akiwa sio mtu wa kujirusha.