Katika mkutano wake huo leo jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine IGP Sirro alionesha hadharani picha za gari ambalo linatajwa kutumika na watekaji hao huku akisema wamegundua liliingia nchini likitokea nchi jirani mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
Katika ukurasa wake wa Twitter na Instagram, Lema ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia CHADEMA, amesema baada ya kumsikiliza IGP Sirro basi yeye kama Waziri Kivuli mwenye jukumu la kuisemea Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia kambi rasmi ya upinzani bungeni atatolea ufafanuzi.
" Nilimsikiliza Mambosasa. Leo nimemsikiliza IGP Sirro katika mkutano wake na wandishi, IGP ameacha maswali mengi yanayoumiza na kuleta hofu kubwa kwa jamii. Kama Waziri Kivuli nitachambua hotuba yake na kuongea na wandishi wa habari katika muda sahihi. Poleni sana famili ya MO Dewji," ameandika hivyo Lema.
