Naandika mada hii ili kushirikishana na wasomaji wangu na jamii kwa ujumla kutokana na mfanano mkubwa wa dalili za Typhoid na Malaria. Wengi hutibu malaria kwa kumeza dawa tu ambapo hupelekea kutokupona kumbe tatizo si malaria bali Typhoid. Na Typhoid ikichelewa kutibiwa huwa ni tatizo zaidi. Kwa hiyo fuatana nami katika mada hii upate kuujua vizuri ugonjwa huu wa homa ya matumbo
DALILI ZA TYPHOID
Homa kali
Kutoka kwa majasho mengi
Kuharisha (bila ya kutoa damu)
Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
Katika wiki ya kwanza:
Joto la mwili huongezeka
Kichwa huuma
Kukohoa
Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Katika wiki ya pili:
Homa huongezeka
Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
Kutapika kwa mgonjwa
Ini la mgonjwa huvimba
Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu:
Matumbo hutoa damu.
Matumbo hutoboka
Wiki ya tatu ikimalizika, homa huanza`kutilia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.
TIBA YA TYPHOID
Mara nyingi haishauriwi kununua dawa kabla ya kujua ni ugonjwa gani unakusumbua hivyo inashauriwa kwenda hospitali au maabara kupima ili kujua tatizo linalokusumbua.
Mara nyingi(NASISITIZA MARA NYINGI) homa ya matumbo haiuwi binadamu. Dawa kama ampicillin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, Amoxicillin and ciprofloxacin hutumika kutibu wagonjwa katika nchi zilizoendelea
KINGA YA HOMA YA MATUMBO
Usafi wa mazingara na wa kibinafsi ni hatua bora ya kujikinga kutokana na ugonjwa huu.
Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hivyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
Homa hii huweza kuenea kwenye mazingara ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Viiliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherixiliyotengenezwa na GlaxoSmithKline