Neymar ambaye aliihama Barcelona misimu miwili iliyopita na kujiunga na PSG katika uhamisho ambao uliweka rekodi ya Dunia amekua akiripotiwa kutokua na furaha kutokana na mwenendo wa klabu yake hiyo haswa katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Ripoti zinasema kwamba Neymar alikua na matarajio ya kushinda mataji makubwa akiwa na PSG ili aweze kujihakikishia nafasi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia lakini mambo yamekua kinyume na matarajio yake.
Mbali na Barcelona kutajwa kumpa nafasi ya kurejea Camp Nou, mahasimu wao na mabingwa wa Ulaya, Real Madrid wanamtazama staa huyo kama mbadala sahihi wa Cristiano Ronaldo ambaye ametimkia Juventus.
