Majaji waaswa kutenda haki kulingana na mazingira


MAHAKAMA imewaasa Majaji nchini kuzingatia sheria  zilizopo kulingana na mazingira ya Taifa na Jamii kwa ujumla katika mchakato mzima wa kutoa maamuzi ili kuweza kutenda haki na usawa.

Wito huo umetolewa na majaji wastaafu wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Jaji Rugazia, John Mjemmas na Agathon Nchimbi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga kitaaluma iliyofanyika mapema leo Oktoba 19.2018  katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Nchimbi amewakumbusha majaji na mahakimu kuhakikisha kuwa  wanakuwa waaminifu wakati wanatimiza majukumu yao kama maofisa wa mahakama ili mwisho wa Siku kila mmoja aweze kuona haki imetendeka.

Amesema, kwa kuwa mahakama ni chombo cha kutoa haki basi ni muhimu kuzingatia sheria zilizopo kulingana na mazingira ya taifa na Jamii katika mchakato mzima wa kutoa haki, Maamuzi yawe ya haki na usawa siyo tu hivyo  bali yaonekane kuwa ya haki na usawa" Amesema Jaji Nchimbi.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items