Kundi la muziki wa Reggae kutokea nchini Jamaica limeachia wimbo wao ambao wamemshirisha msanii Diamond Platnumz.
Msanii mwingine aliyeshirikishwa kwenye wimbo huo unaokwenda kwa jina la Africa x Jamaica ni Stonebwoy kutokea nchini Ghana.
Huu ni wimbo wa pili kwa Diamond Platnumz kufanya na Morgan Heritage baada ya Hallelujah ambao ulitoka September 2017 na kufanya vizuri kwani uliweza kufikisha views Milioni moja ndani ya masaa 15 kwenye mtandao wa Youtube, hadi sasa wimbo huo una views Milioni 10.
Kundi la Morgan Heritagege liliundwa mwaka 1994 na ndugu watano wa msanii wa reggae nchini humo Denroy Morgan, wasanii hao ni Peter Morgan, Una Morgan, Roy Morgan, Nakhamyah Morgan na Memmalatel Morgan. Mwaka 2016 kupitia albamu yao inayokwenda kwa jina la Strictly Roots walishinda tuzo ya Grammy kwenye kipengele cha Best Reggae Album.

Tags:
BURUDANI