NA TIMOTHY ITEMBE TARIME.
MKUU wa wilaya Tarime mkoani Maras,Glorius Luoga ameonyesha kusikitishwa na kushamiri kwa vitendo vya kikatili kwa wanawakje na watotro ikiwemo wanafunzi wa shule za msingi 19 wa halmashauri ya Mji wa Tarime kulawitiwa kwa miaka miwili 2017/2018.
Akiongea katika kikao cha ushauri cha wilaya ambacho kiliambatana na kusoma utekelezaji wa ilani kwa halmashauri za Tarime Vijijini na Halmashauri ya Tarime Mjini kilichowashurikisha wadau mbalimbali wa maendeleo,Luoga alisema kuwa kwa miaka hiyo miwili watoto wa shule wa kiume 19 wamefanyiwa vitendo vya kulawitiwa.
Katikas kikao hicho Luoha aliwataka wanajamii kuungana kwa pamoja ili kutafuta ufumbuzi wa matataizo hayo ili kukomeshwa vitendo wasnavyofanyiwa wanafunzi nyakati za masomo na pindi wakiwa njiani wakienda majumbani kwao.
"Kuna haja jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pamoja na kwa waalimu ili kuhakikisha vitendo vya kikatili vinakomeshwa nimepokea taarifa kutoka halmashauri ya Mji wa Tarime kuwa kuna watoto wa shule 19 wa kiume wamelawitiwa kwa hali hiyo kuna haja jamii kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pamoja na kwa waalimu ili linapotokea tukio kama hili sheria ichukue mkondowake"alisema Luoga.
Kwa upande wake John Ryoba mkazi wa Sirari ambaye pia ni mwenyekiti wa TCCIA Sirari alishauri kuwa kuna haja serikali kutoa elimu ya kupinga vitendo vya kikatili ndani ya jamii ambavyo vinafanywa na baadhi ya watu wasio kuwa na utu vitendo hivyo vikitokea vinaadhiri watoto kisaikolojia na kiakili.
Kwasababu tunakaa mpakani mwa nchi ya kenya na Tanzania ambapo kuna mwingiliano wa makabila kwa hali hiyo wazazi na walezi waelimishwe juu ya mwingilano huo na kuchukua tahadhari kwasababu vitendo vya kikatili vimeshamiri sana hususani vya ubakaji na kulawiti kutokana na mwingiliano wa makabila na vinaadhiri sana jamii.
Ryoba alitumia nafasi hiyo kuitaka halmashauri ya Tarime vijijini kuandaa mpango kazi wa tenda ya ujenzi wa Stendi ya magari inayojengwa huko Ng'ereng'ere ili kuongezxa mapato ya makusanyo ya ushuru kwasababu waliopewa kujenga watu binafsi wameshindwa.
Naye Leonard Daud katibu wa TCCAI alisema kuwa alipata taarifa kuwa watoto waliolawitiwa ni zaidi ya 50 na kuwa watoto hao walitaja waliokuwa wanafanya vitendo hivyo.
"Mimi niombe serikali ifanye uchunguzi kubaini wanaokuwa wanwarubuni watoto wetu wa shule wakiume na kuwafanyia vitendo vya kinyama ili wachukuliwe hatua za kisheria"alisema Daud.