Mbunge wa Kalambo ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kandege, ametaka mpango wa kubomoa nyumba za wananchi usitekelezwe kwanza hadi watakapoandaa makazi mapya.
Alitoa ushauri huo jana katika kikao cha kamati ya ushauri ya barabara mkoani Rukwa.
Naibu Waziri huyo ameutaka Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Rukwa inaposimamia sheria kuzingatia busara pia, kwa sababu tangazo lao limesababisha wananchi kubomoa nyumba zao na kuwaacha katika wakati mgumu.
Alisema lazima wasimamie sheria, lakini kwa kitendo cha kuwapa mwezi mmoja wananchi wawe wamebomoa nyumba walizojenga katika hifadhi ya barabara wakati hawajaandaa mazingira ya ujenzi wa nyumba nyingine, ni kuwasababishia mateso.
Kandege alisema kuwa kama hakuna ujenzi wa barabara unaoendelea, ni vizuri wakapewa muda wa kutosha wananchi waliojenga ndani ya hifadhi ya barabara kwa kuwa hakuna dharura yoyote ili kuandaa makazi mengine, badala yake wawazuie watu wanaojenga nyumba mpya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, alisema kuwa serikali hairuhusu kuvunja sheria, lakini kutokana na bomoabomoa iliyotokea baadhi ya maeneo, iliagiza isimame kwani inaleta athari kubwa kwa wananchi.
Alisema kuwa alishaagiza ubomoaji usimame katika kijiji cha Chala wilayani Nkasi kwa kuwa hakuna ulazima wa kubomoa na hakuna ujenzi wa barabara unaoendelea ili kutosababisha machungu kwa wananchi wa eneo hilo.
Mbunge wa Nkasi Kusini, Ally Kessy, ameitupia lawama mahakama wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa kwa kitendo cha kumruhusu mkandarasi kujenga sehemu ya jengo la mahakama ya mwanzo katika mji mdogo wa Laela katika hifadhi ya barabara na kusema ni kuchezea kodi za wananchi.
Alitoa lawama hizo katika kikao hicho wakati akizungumzia kubomolewa sehemu ya jengo hilo.
Alisema kuwa kuna kila sababu ya kuwachukulia hatua watendaji walioruhusu mkandarasi kujenga jengo hilo wakati walijua lipo ndani ya hifadhi ya barabara kwa kuwa mipaka ya barabara iliwekwa tangu mwaka 1927.
Mbunge huyo alisema kuwa tangu likamilike jengo hilo, limetumika kwa kipindi kisichozidi miaka miwili halafu linabomolewa na kusema huo ni uzembe wa hali ya juu na mkoa hauwezi kupiga hatua.