AT amvaa Vera Sidika kisa Hamisa Mobetto


Msanii wa muziki , AT amekosoa kitendo cha Video vixen, Vera Sidika kuimba muziki, huku akisema video vixen huyo hawezi kuimba na badala yake anapiga kelele.

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya EATV, AT amesema Vera  kutoka nchini Kenya, amimba vibaya na alichokiimba hakieleweki.

“Huyu dada amejikelelesha, video sio mbaya, audio production siyo mbaya, ila muimbaji kaimba vibaya, hakieleweki kinachoimbwa ni nini, hajatayarishwa wala hajajitayarisha kuwa msanii, inawezekana kaona tu Mobetto alitoa kazi yake na yeye akaona atengeneze, kuimba sio kujamba kila mtu anaweza, lazima heshima iwekwe mezani, hizo kelele ni mbaya, mimi siwezi kuita nyimbo”, amesema AT.

Siku chache zilizopita Vera Sidika ameachia wimbo wake wa kwanza ambao inadaiwa amemuimba aliyekuwa mpenzi wake Otile Brown unaojulikana kwa jina la 'Nalia'.