Benson Chonya
Ili kuweza kufikia lengo lolote maishani ni lazima uwe na Nidhamu binafsi bila kuwa na nidhamu huwezi kuwa makini katika kutimiza lengo lolote lile maishani hata liwe dogo kiasi gani.
Nidhamu binafsi ni ule uwezo wa kuweza kujitawala wewe mwenyewe, kiasi kwamba unaweza kujizuia baadhi ya vitu unavyovipenda ili kuweza kutimiza lengo fulani ulilojiwekea siku za baadae, kwa mfano kujizuia kula vyakula vya mafuta au sukari nyingi hata kama unavipenda ili uwe na afya nzuri baadae au uwe na mwili mzuri.
Pia nidhamu binafsi ni pamoja na kujiwekewea sheria zako wewe mweyewe, taratibu na mikakati na kuhakikisha unaifuata siku zote za maisha yako. Kwa mfano unajiwekea utaratibu kwamba kwenye maisha yangu sitajihusisha na mahusiano ya kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja na kuhakikisha ni kweli hujihusishi na hizo tabia hio ndio nidhamu binafsi.
Pia nidhamu binafsi ni muhimu kujijengea hasa pale unapotaka kuacha baadhi ya tabia mbaya ulizonao ambazo unaona hazifai kwa mfano kuvuta sigara na unataka kuacha kuvuta sigara
Kuna mwanasaikolojia mmoja aliilezea kama “disclipine is freedom” ,unaweza kukataa hio maana lakini ukifikiria kwa undani ni kweli, kwa mfano unakuta mtu anataka kuwa na mwili uliojengeka kimazoezi lakini hana nidhamu ile ya kufuatilia mazoezi hivyo huyo mtu anakuwa ana mwili ambao haupendi.
Pia nidhamu ni kuweza kufanya yale unayoyafikiria kuliko unayoyahisi,mara nyingi ni kujitoa muhanga kutofanya yale unayoyapenda yasiyo na faida kwako kama kuangalia movie kutwa nzima na kufanya yale yaliyo ni muhimu katika maisha yako mfano kupenda kusoma mambo mbalimbali mbali ili kukuza ufahamu na uelewa wako.
