Watu nane wameripotiwa kufa kwa kuteketea kwa moto na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya gari mbili aina ya Hiace zilizogongana uso kwa uso na kusababisha gari hizo kuungua kwa moto na kuteketea. Ajali hiyo imetokea majira ya 9:30 Alasiri kwenye Kijiji cha Komaswa wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Kamanda Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Henry Mwaibambe amesema kuwa hadi sasa idadi kamili ya watu waliokufa katika ajali haijajulikana ila taarifa za awali zinasema watu wanane wamefariki kutokana na ajali hiyo huku Chanzo cha ajali bado hakijajulikana


