Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema kamwe Serikali ya Tanzania haitaruhusu ushoga kwasababu nchi hii ni hekalu la roho Mtakatifu haiwezi kuruhusu mambo machafu na kwamba kila kiungo kilichoumbwa na Mungu kwenye mwili wa mwanadamu kina kazi yake.
Lugola ametoa kauli hiyo bungeni wakati akitolea ufafanuzi kuhusu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Konde, Khatibu Haji aliyoitoa wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/20.
"Hawa mashoga anaowazungumzia ambao ni binadamu wenye viungo mbalimbali vya mwili, viuongo ambavyo mashoga wanavitumia vina kazi maalum kwa mujibu wa uumbaji Mwenyezi Mungu, serikali yetu kamwe haitaruhusu mwanadamu yeyote kubadili matumizi ya kiungo ambacho kimekusudiwa kwaajili ya kutolea haja kitumike katika matumizi mengine ambayo Mungu hakukusudia," amesema Kangi Lugola.
"Kwahiyo nimempa taarifa serikali yetu inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kwanza tuna kanuni zenu za sheria na adhabu inazuia makosa inayoitwa unnatural offences kwahiyo yanazuia kubadilisha matumizi ya kiungo kwa mwanadamu, kwahiyo asiseme serikali inajichanganya juu ya jambo hili ni melekezo ambayo tunayatoa mabavyo huenda vyombo vinaandikwa tofauti Tanzania ni hekalu la roho mtakatifu, hatuwezi serikali kukubali hekalu la roho mtakatifu likatumika kwa mambo machafu ambayo hayakubaliki," alisisitiza Lugola huku Wabunge wakimpigia makofi.