BAADHI ya wafanyabiashara wanaotoa mifugo Babati kwenda Kenya kupitia mpaka wa Namanga, wilayani Longido, wamelalamikia kutozwa mara mbili ushuru wa mifugo.
Wakizungumza katika operesheni ya kudhibiti usafirishaji wa mifugo na chakula ndani na nje ya nchi inayosimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi mkoani hapa juzi, wafanyabiashara hao walisema pamoja na kutozwa ushuru mara mbili pia wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa katika vizuizi.
Mfanyabiashara Sanimo Lukas, amesema kumekuwa na tatizo kubwa la kusumbuliwa na askari sehemu za vizuizi ambavyo pia wamekuwa wakidaiwa fedha huku wakiwa tayari wamelipia kila tozo toka watokako.
Alisema anashangazwa na Serikali kwa kile wanachokifanya kwani kumekuwa na tozo mbili ambazo wamekuwa wakilipa.
“Tunalipia tozo ya Sh. 1,500 wakati wa kununua mbuzi tukiwa mnadani na Sh. 7,500 kwa ajili ya kibali cha usafirishaji kwa kila mbuzi lakini tunashangaa tukifika mpaka wa Namanga tunaambiwa tushushe mbuzi tulipe tena upya Sh. 1,500, tunashindwa kuelewa ni ya nini, haiwezekani mbuzi mmoja ulipie ushuru mara mbili wakati tulishalipia tozo zote.
"Tunaiomba serikali ituangalie pale mpakani kwenye soko la Namanga na kwenye vizuizi watuangalie, maana askari wanatusumbua sana, sisi hatuna kazi ya kufanya, kazi tunayotegemea ni kufanya biashara ya usafirishaji, hatulimi sasa kama tutakuwa tunadaiwa kila geti fedha, tutashindwa kufanya biashara hii,” alilalamika.
Katika operesheni hiyo, zaidi ya sh milioni 300 zilipatikana.
Lakini kwa upande wao wafanyabiashara hao walisema zoezi la usafirishaji wa wanyama nchini kenya ni nzuri kuliko Tanzania kwani wakifika mpakani mwa Kenya na Tanzania wakitaka kuingiza mifungo yao Kenya hutoa Sh. 125, 000 kwa ajili ya kuingia nchini humo na baada ya hapo hawadawi tozo yoyote baada ya kulipia fedha hizo tofauti na upande wa Tanzania.
Walisema kwa upande wa Tanzania, wanasimamishwa na askari njiani zaidi ya saa nzima kitu ambacho kinahatarisha maisha ya wanyama kwani wakisimama muda mrefu kwenye gari kwa kuwa wanakuwa wamebanana hukosa hewa na hivyo kusababisha kufa.
“Tukishalipa hiyo fedha njiani hakuna cha askari wala nani anaetudai fedha njiani, zaidi ya kuulizwa kibali cha usafirishaji hata kama unaenda wapi ndani ya nchi hiyo tofauti na huku kwetu kila geti askari wanataka fedha,’’ alisema.
Alisema suala la askari barabarani wanaowakwaza wasafirishaji tayari wameongea na uongozi wao polisi kwani zoezi hilo wanasaidiana na kamishina wa polisi hivyo wamewaomba wafanyabiashara kuendelea kushirikiana kwa ajili ya kuitoa sekta mahali ilipo na kwenda mbele na hivyo itasaidia sekta hiyo kuonekana kuwa na mchango mkubwa serikalini.