Msanii wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amefunguka mara baada ya baadhi ya wasanii kuanza kuandaa show zao wenyewe.
"Kuna umuhimu kwa sababu inapotokea mtu mwingine hawezi kukupa kazi wewe mwenyewe unaweza kujipa kazi lakini si kila msanii anaweza akaandaa show na sio kila msanii anaweza akafanya show akajaza," amesema Lady Jaydee.
"Kwa hiyo kuna tofauti hapo na wasilaumiwe watu ambao hawawezi kuandaa show lakini ni jambo zuri kwa sababu tutawapa hata waandaaji changamoto kuwa wasituchukulie poa," amesema kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM .
