Msanii wa muziki Bongo, Lady Jaydee amesema kuwa kila nchi ina sheria zake hivyo yeye hawezi kuimba wimbo ambao Basata watamuuliza kwanini ameimba hivyo.
Kauli hiyo ya Lady Jaydee imekuja baada ya kuhojiwa kuhusu baadhi ya wasanii kuitwa Basata ambapo amesema kuwa watu wanapenda sana muziki ila inabidi wawe makini katika uimbaji huo.
"Unajua kila nchi wana sheria na wanaweka vyombo vyao ambavyo vinaweka sheria zao ambavyo vinakataza vitu fulani na kukubaliana na vitu fulani , mimi huwa naogopa kuongelea ishu za watu saa zingine mtu anaweza kusema kwanini umesema hivi akatafsiri tofauti sana," amesema Lady Jaydee Time FM.
"La msingi naweza kusema mimi siwezi kufungiwa na Basata mi siwezi kuimba wimbo wowote ambao wataniuliza kwanini umeimba hivyo na sijawahi kuitwa niitwe kufanya nini kwahiyo nafikiri tu tuwe makini katika hii kazi watu wanapenda miziki na nini lakini tuangalie pia."
Lady Jaydee kwasasa anatamba na kibao wa wimbo wake mpya unaoitwa 'Boyfriend wa Dar es Salaam'
